Wakati Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijana wilayani Kahama mkoani Shinyanga ikiadhimisha miaka 12 tangu kuanzishwa kwake Wilayani humo ikiwa ni miaka 25 tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo nchini Tanzania, Huduma hiyo imeiomba serikali kupewa nafasi na kutambuliwa katika vyuo vya serikali
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo ameeleza changamoto inayoikabili huduma hiyo ikiwa ni changamoto ya kukosa nafasi katika vyuo vya serikali ambapo wameiomba Halmashauri hiyo kuwatambua na kuwawezesha katika kipindi cha vyuo
Katika kujibu risala hiyo Mgeni Rasmi bi Swahiba Chem chem ambaye ni Afisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii manispaa ya Kahama akimuwakilisha Mkurugenzi wa manispaa ya kahama ameeleza kuwa Halmashauri ina ufadhiri wa wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu hivyo waainishe watu wanaohitaji ufadhili na kuwasilisha Halmashauri kwa ajili ya usaidizi
Baadhi ya vijana ambao ni zao la shirika hili wamesema kuwa shirika hili limewajengea uwezo kupitia fani mbali mbali ikiwa ni pamoja na upigaji picha, ushonaji wa nguo, pamoja na upakaji rangi ambazo zinawasaidia kujiingizia kipato
Huduma ya mtoto na maendeleo ya Kijana Tanzania inaratibiwa na Shirika la compassion Tanzania ambapo kwa kahama limetimiza miaka 12 na linahudumia watoto takribani 1200 wilayani Kahama.




