Watu watatu wamejeruhiwa hadi kunusurika kifo baada ya nyumba ya ofisi waliyokuwemo kushambuliwa na wachimbaji wadogo wa mgodi wa Mwakitolyo namba 5 wilaya ya Shinyanga vijijini Mkoani Shinyanga.
Watu hao ni watu wenye asili ya China wawili pamoja na Mkalimani wao.ambaye ni mtanzania aliyefahamika kwa jina la.dr Ben kutokea Dodoma ambapo walishambuliwa wakiwa katika ofisi ya wachimbaji wadogo wa Dhahabu katika mgodi huo baada ya kuonekana katika eneo hilo bila pasina kuwa na taarifa kwa wachimbaji hao pamoja na uongozi wao hali iliyozua taharuki kwa kudhani kuwa eneo hilo linaenda kuuzwa kwa wachina hao hivyo kuwafanya wachimbaji hao kuivamia ofisi na kuishambulia kwa mawe na kuchoma pikipiki iliyokuwa nje ya ofisi hiyo
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Benedicto Robert amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa chanzo siyo hao raia wa kigeni kuwepo katika eneo hilo, bali chanzo ni kuingia katika eneo hilo pasina taarifa kwa wachimbaji hao kwani kitendo hicho kilizua taharuki kutokana na kile kilichoshuhudiwa katika migodi ya jirani mpaka kupelekea kupewa wawekezaji wengine badala ya wazawa
Kwa upande wake Meneja wa mgodi huo Matemla Michael Amesema kuwa licha ya kuharibiwa kwa mali zenye thamani ya zaidi ya milion 30 wachimbaji hao wanamiliki Leseni za uchimbaji katika eneo hilo ambapo ametumia fursa hiyo kuiomba serikali iendelee kutoa elimu kwa watanzania juu ya utaratibu na namna ya kufika katika maeneo mbali mbali ili kuepuka taflani katika maeneo mbali mbali. Michael pia amesema kuwa mgodi huo unajumuisha wachimbaji zaidi ya elfu 30 ambao wanategemea mgodi huo kujipatia mahitaji yao ya msingi ya kila siku
Kwa upande wao baadhi ya wachimbaji ambao hawakupenda majina yao yatambulike wamesema kuwa hawako tayari kuuachia mgodi huo uende kwa wawekezaji kwani ndio uliobaki ambao unawanufaisha wazawa wa eneo hilo na kusema kuwa watatumia nguvu zote.kuulinda mgodi huo ambapo katika Hali hiyo hiyo baadhi yao wameiomba serikali kuweka Utaratibu mzuri wa kimaelewano kama wanahitaji kuweka muwekezaji mwingine
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga kupitia ofisi ya RPC lilipotakiwa kutoa ufafunuzi juu ya hili limesema kuwa limeshatoa taarifa kwa vyombo vya habari ambayo taarifa hiyo nimeitafta bila mafanikio.





