Na Mubali Junior
Mmoja wa watu waliofunikwa na vifusi vya jengo la ghorofa tano lililobomoka na ambaye yupo hai katika ghorofa ya chini ya jengo hilo, Delvin Safels msichana mwenye umri wa miaka 29, ameendelea kuwasiliana na wazazi wake pamoja na mchumba wake, akiwaeleza mateso anayopitia kutokana na mguu wake na mkono wake kubanwa na vifusi vya jengo hilo huko chini aliko
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akiwatumia ujumbe wa sauti wazazi wake na mpenzi wake, akiwaambia jinsi anavyowapenda.Lakini pia anawaeleza kuwa anapitia maumivu makali ya mkono na mguu wake vilivyobanwa na vifusi pamoja na baridi kali na na giza totoro huko aliko.
“Ninaamini mwanangu atatoka akiwa hai,” Dion baba yake mzazi binti huko akijifariji kwa uchungu Baba mzazi wa msichana huyo amekuwepo katika eneo hilo tangu siku ya Jumatatu, akiwa na matumaini ya mtoto wake kupatikana akiwa hai. “Ni kijana mwenye nguvu, nadhani ataokolewa usiku wa leo au hivi karibuni.”Aliongeza.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Afrika kusini, waokoaji bado wanawatafuta watu 41 ambao bado hawajulikani walipo katika eneo hilo la Pwani ya kusini ya mji wa George.
Kwa mujibu wa taarifa za Manispaa ya mji wa George kulikuwa na wafanyakazi 75 wakati jengo hilo lilipoanguka. Chanzo cha kuporomoka ghorofa hilo lililokuwa likiendelea kujengwa bado kinachunguzwa.
NINI KINAENDELEA KATIKA HARAKATI ZA UOKOAJI?
Kikosi cha waokoaji wapatao 200 wakiwa na mbwa maalum wa kunusa wakiwa na vifaa maalum vya kunyanyua vitu vizito kama vile matofali,nondo na zege huku wengine wakitoa kwa mikono ili kuweza kuwapata watu walionaswa kwenye vifusi vya jengo hilo.
Juhudi za uokoaji zinajumuisha watu 200 walio na mbwa wa kunusa, vifaa vya kunyanyua vizito na msako wa kuondoa matofali ya zege na uchafu kwa mikono, shughuli nzima ya uokoaji inatarajiwa kuchukua kati ya siku nne ama tano.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alikaririwa na vyombo vya habari nchini humo akisema kuwa anaungana na familia zilizopoteza wapendwa wao katika wakati huu mgumu na kuagiza uchunguzi wa kina kufanyika ili tukio kama hili lisijirudie