TMA WATABIRI KIMBUNGA KINGINE IALY, ILA HAKITAKUWA NA MADHARA TANZANIA | Extra Mile

Saturday, May 18, 2024

TMA WATABIRI KIMBUNGA KINGINE IALY, ILA HAKITAKUWA NA MADHARA TANZANIA

  Extra Mile       Saturday, May 18, 2024

 

Mamalaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imeotoa taarifa ya utabiri wa uwezekano wa kutokea kimbunga kingine kijulikanacho kama Ialy.

Kwa mujibu wa TMA kimbunga hicho Ialy kinajitengeneza katika eneo la kaskazini mwa bahari ya Hindi katika eneo hilo la kisiwa cha Madagascar.

Katika taarifa ya TMA ya TMA iliyotolewa May,17,2024 ni kwamba mwenendo wa hali ya hewa unaashiria Kimbunga hicho kitaendelea kusalia ndani ya bahari ya Hindi kati ya Madagascar na Ushelisheli ndani ya siku nne kabla ya kuanza kupoteza nguvu zake.

JE KIMBUNGA IALY KITAKUWA NA MADHARA?

Muonekano wa Mawimbi makubwa ndani ya Bahari ya Hindi.Picha na https://pixabay.com/photos/sea-wave

Kutokana na umbali uliopo kati ya nchi ya Tanzania na eneo ambalo Kimbunga hicho kitaanzia,Mamlaka imesisitiza kuwa hakuna madhara yoyote yanayotarajiwa kama vile ongezeko la mvua,japo kuwa vipindi vya upepo mkali na mavimbi vitakuwepo ndani ya bahari ya Hindi.

Watumiaji wa Bahari ya Hindi na jamii kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa kutoka TMA lengo la kupata miongozo mbalimbali ya kitaalam.

Hata hivyo Mamlaka hiyo katika taarifa hiyo imeuhakikishia umma kwamba inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa Kimbunga hicho na madhara yanayoweza kutokea kama yapo.

logoblog
Previous
« Prev Post