NA JOHN ISRAEL, DODOMA
IMEELEZWA kuwa Tanzania ni nchi pekee Duniani iayotoa cheti cha Ndoa kwa wanandoa Bila wahusika kuwa na Elimu Stahiki hali inayosababisha ndoa nyingi kuvunjika mahakamani hasa za wakristo.
Hayo yameelezwa februari 11,2026 na Katibu Mkuu wa Huduma ya 2=1 Ministries Tanzania, Askofu Dkt. Burton Saulo Yuda kwenye kongamano la wanandoa, wanaojiandaa kuingia katika ndoa na wajane lililofanyika kwa siku mbili katika kanisa la PRA Jijini Dodoma
amesema 2=1 imekuja kuponya ndoa na kanisa la Tanzania kwani nchi hiyo ndiyo nchi pekee inayotoa vyeti vya ndoa bila wahusika kuwa na elimu ya kada hiyo nyeti ambayo ni chanzo cha kila kitu kwenye familia, Jamii, Taifa na Dunia kwa ujumala
Dkt. Yuda amesema kuwa wakati alipokuwa akichukua shahada ya Udakitari alibaini kwenye nchi 17 alizofanya utafiti kwenye eneo la uhusiano kuwa ndoa hasa za wakristo wakiwemo viongozi wa dini hiyo zinaongoza kuvunjwa mahakamani.
“ni Tanzania pekee inayotoa cheti bila wahusika kumaliza mafunzo kwenye kada ya ndoa ambako wahusika hufika madhabahuni wanavalishana pete, kwa maneno machache ya msajili wa ndoa hiyo kisha wanakabidhiwa vyeti bila hata kujua kwenye ndoa kuna nini
Adha amesema elimu nyingine zote lazima mtu asome afanye mtihani afaulu ndipo apate cheti husika lakini kwenye Ndoa si hivyo
‘’nilipokuwa nikifanya utafiti wakati nilipokuwa nikichukua shahada ya yangu ya udaktari, katika nchi 17 za Africa niligundua, Ndoa zinazoongoza kuvunjwa mahakamani ni za wakristo huku wengi wao wakiwa viongozi wa dini hiyo wakiwemo maaskofu, wachungaji, wazee wa kanisa na wengine’’, amesema
Akiongea kwenye kongamano hilo Mkurugenzi wa 2=1 Ministries Africa Gavin Moses na Ammelia moses amesema ili amani na usalama viwepo kuanzia ngazi ya familia, jamii, Taifa na Dunia kwa ujumla ndoa zote zinamhitaji Mungu.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa 2=1 Ministries Tanzania Askofu Amos amesema huduma hiyo imezaliwa upya, kwani awali watu waliaminishwa kuanzishiwa Miradi bila kupewa maarifa, lakini sasa maarifa kwanza ndipo miradi ifuate.
Katika kongamono hilo lililoongozwa na Mkurugenzi wa huduma ya 2=1 Africa Gavin na mke wake Ammelia kutokea nchini Africa Kusini, pia ulihudhuriwa na maaskofu nane toka nchini Congo DRC, ambapo uongozi wa taifa la Tanzania umewasisitiza washiriki wote kuwa watapata maelekezo ya hatua zitakazofuta kutoka kwa viongozi wa mkoa wa Dodoma unaoongozwa na Askofu Dkt. Elia Mauza.