Mwamuzi wa kati Nassoro Mwinchui kutoka mkoani Tanga amekabidhiwa Dabi ya Yanga na Simba inayotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar Jumapili Machi 1, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan.
Kwa mujibu wa ratiba ya waamuzi iliyotolewa leo Ijumaa Februari 27, 2026, pambano hilo linatarajiwa kuchezwa saa 2:15 usiku huku Mwinchui akisaidiwa na waamuzi wasaidizi Kassim Mpanga (Dar es Salaam) na Hamdan Saidi (Mtwara).
Mwamuzi wa akiba katika mchezo huo atakuwa Ramadhan Kayoko (Dar es Salaam).
