Bonanza la Michezo Halmashauri ya manispaa ya kahama Mkoani Shinyanga limefanyika leo katika kiwanja cha Manispaa ya kahama (Uwanja wa Taifa) likiwa na lengo la kuhamasisha amani, Mshikamo, na umoja ili kujenga Tanzania imara.
Bonanza hilo limepambwa na michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu, mchezo wa mpira wa nyavu, mchezo wa kukimbiza kuku, mchezo wa mikono (handball) na michezo mingine kwa lengo la kuimarisha afya, kujenga umoja na mshikamano pamoja na kuimarisha ushirikiano miongoni mwa washiriki.
Akizungumzia bonanza hilo Mkuu wa kitengo chaUtamaduni, Sanaa na Michezo amesema bonanza hilo limezikutanisha Halmashauri ya Manispaa ya Kahama (mwenyeji), Halmashauri ya Wilaya ya Igunga pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Baadhi ya Musa Joseph Makandiro kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na Tausi Kisanzo kutoka Manispaa ya Kahama wametumia bonanza hilo kuwa rai vijana kutumia majukwaa ya kimichezo ili kuepuka makundi yanayoweza kuasisi tabia zisizofaa kwenye jamii na kuleta athari hasi kwa jamii.
"Bonanza hili ni jukwaa muhimu kwa vijana kutumia michezo kuimarisha mshikamano, kujenga umoja na kuepuka tabia zisizofaa zinazoathiri jamii," alisema Musa Joseph Makandiro wa Wilaya ya Maswa.