MAAFISA LISHE WATOA ELIMU YA UANDAAJI WA CHAKULA CHA WATOTO - KAHAMA | Extra Mile

Friday, April 3, 2026

MAAFISA LISHE WATOA ELIMU YA UANDAAJI WA CHAKULA CHA WATOTO - KAHAMA

  Extra Mile       Friday, April 3, 2026


Na Kahama MC

 Maafisa Lishe wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama  Waadhimisha siku ya Afya na Lishe ya Kijiji (SALIKI) kwa kuendesha mafunzo ya uandaaji  na kupika vyakula vya watoto wadogo.

Mafunzo hayo ya Vitendo yalifanyika Kwenye Zahanati ya Isagehe Iliyopo Kwenye Kata ya Isagehe.

Mafunzo hayo ni Shughuli inayohusisha Vijiji na mitaa yote ya Manispaa ya Kahama ambayo huadhimishwa  mara moja Kwa kila robo ya mwaka.

Akiongoza Mafunzo hayo Kaimu Afisa Elishe wa Manispaa ya Kahama Bw. Andrew Zebedayo Kasuka amesema kuwa 

Shughuli hii hufanyika kwenye Vijiji na Mitaa yote na Shughuli kuu zinazofanyika kwenye siku hii ni pamoja na

Upimaji wa Hali ya Lishe Kwa watoto wa chini ya miaka mitano, Utoaji wa elimu ya Afya na Lishe Kwa wazazi na walezi wa watoto wenye chini ya miaka 5,  Kufanya maonyesho ya jiko darasa Kwa  kuwafundisha wazazi na walezi namna ya kuandaa na kupika chakula Cha watoto wadogo.







logoblog
Previous
« Prev Post