Na mwandishi wetu,Dodoma
Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Patrobas Katambi ameahidi kuwa Jeshi la zimamoto na uokoaji kwa mwaka 2026/27 litaendelea kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi zaidi ili kupunguza madhara yatokanayo na moto na majanga mengine kote Nchini Tanzania ikiwa kwa kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili 2026 limezima moto na kufanya uokoaji katika matukio 4,436, ambapo majeruhi 1,713 waliokolewa
Ameyasema hayo Mei 25, 2026 Bungeni Mjini Dodoma wakati Waziri Katambi akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka 2026/2027, akisema pia kuwa hadi kufikia Aprili 2026, Wizara kupitia Jeshi la Zimamoto na uokoaji imefanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto na majanga mengine katika maeneo 62,100, jumla ya shilingi Bilioni 12.29 kikikusanywa sawa na asilimia 98.38 ya lengo lililowekwa.
"Katika mwaka 2026/27 jumla ya maeneo 110,000 yatakaguliwa na Shilingi bilioni 17 zinatarajiwa kukusanywa." Amesema Waziri Katambi.
Waziri Katambi pia anesema kutokana na uhitaji mkubwa wa mabomba maalumu ya kuchukulia maji ya magari ya kuzima moto (fire Hydrants) hasa katika ngazi ya Wilaya na Halmashauri, Jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kushirikiana na mamlaka za maji, linatekeleza mpango wa miaka mitano kwaajili ya kufunga mabomba (fire Hydrants) 4,256 katika ngazi za Wilaya zitakazowezesha upatikanaji wa maji ya kuzima moto.
Aidha amesema kwamba Wizara kwa kushirikiana na Jeshi la zimamoto na uokoaji inaendelea na ukamilishaji wa vituo saba vya zimamoto na uokoaji Nchini ambapo hadi kufikia Aprili 2026, ujenzi wa Vituo 2 umekamilika huko Njombe na Simiyu na umaliziaji unaendelea katika Mikoa ya Manyara, Katavi, Geita, Kagera na Songwe.
Ameeleza pia kwamba Jeshi hilo limepokea Shilingi Bilioni 2.46 kwaajili ya ujenzi wa vituo vya Zimamoto na uokoaji katika Wilaya za Bunda, Gairo, Nzega na Sengerema pamoja na kwenye Halmashauri za Chalinze na Mafinga na kufanya ukarabati wa kituo cha Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Ruvuma. Aidha, katika mwaka 2026/2027 Shilingi bilioni 10.6 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo saba (7) vya Zimamoto na Uokoaji katika Mikoa ya Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza, Pwani na Shinyanga.