Mafunzo haya yalianza rasmi tarehe 17 na kuzinduliwa rasmi tarehw 18 katika shule ya Msingi Kahama ambapo walimu 35 kutoka shule mbali mbali hapa manispaa ya Kahama na mikoa jirani walishiriki
Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilayani kahama Hussein Salumu amesema kuwa watahakikisha wanawawezesha walimu hawa ambao wamepata mafunzo kutumia kile walichojifunza
Na Samuel Samsoni
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha wanakifanyia kazi walichojifunza atahakikisha hakuna mwalimu yeyote atakayesimama kwenye benchi kama hana cheti cha mafunzo yoyote ya ukocha
Mgeni rasmi wa hafla hiyo bwana Festo Ntibabala ambaye ni mkuu wa kitengo cha sanaa na michezo hap Manispaa ya Kahama amesema kuwa kama serikali imejipanga kuhakikisha wanakuza soka nchini kuanzia ngazi za chini na hizi ni jitihada mojawapo zinazofanywa na TFF na kuwaahidi kufanya zaidi ya hapo katika manispaa hiyo
Baadhi ya Wahitimu wa mafunzo hayo akiwemo Aisa Godson na Hamad Sule wamesema kuwa kuwepo kwa mafunzo hayo kumebadilisha mitazamo ya ufundishaji wa mpira wa miguu na kusema kuwa inaenda kuleta chachu na mabadiliko katika soka la manispaa ya Kahama.







