Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Aikael Mbowe ameongoza maandamano yaliyoitwa maandamano ya amani ambayo yaliangazia mambo mbali mbali katika jamii
Na Samuel Samsoni
Maandamano haya ya amani yaliongozwa na mwenyekiti huyu huku akisema kuwa lengo la.maandamano haya siyo kuoneaha utimamu wa waandamanaji kwamba wanaweza kutembea bali ni kuonesha hisia zao za namna ambavyo serikali inawaumiza
Aidha maandamano hayo yaliwahusisha mamia ya waandamanaji wakiandamana kutokea Kata ya Mwendakulima Halmashauli ya Kahama Manispaa ambapo ndipo ulipofanyika mkutano wa hadhara hapo. Katika safari hiyo ya maandamano mabango mbali mbali yalioneshwa huku yakibeba hisia za waandamanaji
Hata hivyo katika mkutano wa hadhara Mbowe amesikika akisema kuwa wao wamejipanga kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki kuanzia ngazi zote za uongozi huku akitoa wito kwa jeshi la polisi kulinda haki katika kipindi chote cha upigaji kura.
Baadhi ya wananchi wamesema kuwa licha ya maandamano haya bado hawana matumaini ya kwamba mandamano haya yana tija yoyote katika kile ambacho wao wamekifikiria kama waandamanaji.







