Na Mapuli Kitina Misalaba
Wazazi, walezi na jamii wameshauriwa kuendelea kuwalea watoto katika misingi ya mila na desturi ili kuimarisha utamaduni wa kila kabila na kuepukana na mmomonyoko wa maadili hapa nchini.
Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wazee wakazi wa Himaya ya Busiya iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, wakati wakizungumza na Misalaba Media.
Wamesema mmomonyoko wa maadili hasa kwa vijana unatokana na malezi mabaya yanayoanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla ambapo wamesema ni vema wazazi kuwafundisha watoto mila na desturi za kabila husika ili kuwaepusha na tabia za kuiga mila za kigeni.
Pia wameishauri serikali nchini kuwapa kipaumbele wazee na viongozi wa kimila katika hatua za kutokomeza mmomonyoko wa maadili.
Wamesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikuwa ikiwemo vijana kuwaepusha na makundi mabaya yanayopelekea mmomonyoko wa maadili, vitendo vya ukatili na ndoa za utotoni.