KISA TENDO LA NDOA, ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKEWE | Extra Mile

Friday, February 20, 2026

KISA TENDO LA NDOA, ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKEWE

  Extra Mile       Friday, February 20, 2026







Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani



Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Busu Lugwisha(51) mkazi wa Kijiji cha Masigo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumuua mke wake aitwaye Regina Thobias (40) kwa kumpiga na kitu kizito chenye mcha kali kichwani baada ya kunyimwa tendo la ndoa na mkewe kwa muda mrefu.




Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Busu Lugwisha(51) mkazi wa Kijiji cha Masigo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumuua mke wake aitwaye Regina Thobias (40) kwa kumpiga na kitu kizito chenye mcha kali kichwani baada ya kunyimwa tendo la ndoa na mkewe kwa muda mrefu.


Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amesema tukio hilo la mauaji hayo ya kusikikisha limetokea Februari 19 majira ya saa kumi usiku nyumbani kwa wanandoa hao wawili waliokuwa wakiishi wakiwa mume na mke .


Kamanda Ngonyani amesema chanzo cha mauaji hayo ya mwanamke huyo kilitokana na wivu wa mapenzi kwa kile kunachodaiwa ni hasira zamthumiwabaada yakunyimwa tendola ndoa na Ragina Thobias ambae alikuwa ni mke wake .


Amefafanua kuwa kutokana na wivu huo wapenzi ndio ulimfanya mtuhumiwa Busu kumpiga kichwani na kitu kizito kichwani upande wa kisogoni na kumsababishia mkewe kufa hapo hapo .


Ameeleza kuwa katika mahojiano ya awali na mtuhumiwa jeshi la polisi limebaini mauaji hayo yametokana na wivu wa mapenzi baada ya mtuhumiwa kukiri kufanya mauaji hayo kwa kile alichodai kuwa mkewe alikuwa amenyima tendo la ndoa kwa muda mrefu sasa .


Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika kituo cha afya cha Inyonga B kwa ajiri ya uchunguzi zaidi na mara uchunguzi utakapokuwa umekamilika watakabidhiwa ndugu wa marehemu kwa ajiri ya mazishi .


Kamanda Ngonyani amesema mtuhumiwa bado anaendelea kushikiliwa na polisi na mara upelelezi ukikamilika atafikishwa mara moja mahakamani ili akajibu tuhuma zinazo mkabili .


Jeshi la Polisi linatowa wito watu waache tabia ya kujichukulia sheria mikononi na badala yake wawasilishe changamoto zinazowakabili kwa viongozi wao wa familia dini mitaa au mamlaka za kisheria kwa ajiri ya utatuzi .

logoblog
Previous
« Prev Post