
Na Mwananchi Digital
Wanawake wa Kijiji cha Kilimampimbi, Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, wametangaza kususia kubeba mimba na kuzaa kama njia ya kushinikiza Serikali kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho uliokwama tangu mwaka 2014.
Uamuzi huo umetolewa mara kadhaa katika mikutano ya kijiji, ambapo wanawake hao wameeleza kuwa hawapo tayari kuendelea kubeba jukumu la uzazi huku wakikosa huduma za afya karibu na makazi yao.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Daud Mwalwanda, akizungumzia msimamo huo, amekiri kuwepo kwa tishio hilo na kusema kuwa malalamiko ya wanawake yamekuwa yakiwasilishwa mara kwa mara katika mikutano mbalimbali ya kijiji kwa muda mrefu.
“Bado hatuwezi kusema kama msimamo wao unaweza kufanya kazi, lakini mara kadhaa kwenye mikutano wamekuwa wakieleza hilo, ingawa inaweza ikawa ni kauli tu, bila kujali mazingira na uhalisia wake,” amefafanua Mwalwanda.
Amesema Kijiji cha Kilimampimbi chenye vitongoji vinne na wakazi 540 hakina kituo cha kutolea huduma za afya, hali inayowalazimu wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma katika vijiji vya Msamba na Ikomela au hadi Hospitali ya Wilaya ya Mbozi.
Mariam Mtafya, mmoja wa wanawake wa kijiji hicho, akizungumza kijijini hapo, amesema uamuzi wao unatokana na mateso wanayopitia wanapohitaji huduma za uzazi.
Soma zaidi kwenye Tovuti ya Mwananchi
#mwananchiupdates
Friday, February 20, 2026
Home » » WANAWAKE MBOZI WATISHIA MGOMO WA KUTOBEBA UJAUZITO
WANAWAKE MBOZI WATISHIA MGOMO WA KUTOBEBA UJAUZITO
Extra Mile Friday, February 20, 2026
Previous
« Prev Post
« Prev Post
Next
Next Post »
Next Post »