Chanzo: Kahama Manispaa
Kampeni ya Kitaifa ya Uhamasishaji na utoaji wa Chanjo ya Matone ya Polio awamu ya kwanza kwa watoto wenye umri chini ya miaka kumi (10) kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama imeanza rasmi leo Machi 24 kwa Wataalamu wa Afya kupita nyumba kwa nyumba, vituo vya kutolea huduma za afya, maeneo maalum yenye mikusanyiko ya watu wengi kama vile: vituo vya kulelea watoto wadogo shule zote za msingi, makao ya watoto, stendi za mabasi, masoko na minada.
Akizindua zoezi hilo Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama Bw. Hery Sylivester amesema kuwa Manispaa ya Kahama imepokea dozi laki moja themanini na mbili na mia tatu (182,300) ambazo zitakumika kuwa fikia walengwa laki moja arobaini na tano elfu na mia nane ishirini (145,820).
Aidha amesema kuwa chanjo hiyo haina Madhara yoyote kwa Watoto na amewataka Wananchi wote kuwapa ushirikiano Wataalamu hao ili kufanikisha zoezi hilo.
Utoaji wa Chanjo hiyo umeanza rasmi leo na utarajiwa kuhitimishwa Machi 27, 2026.



