Na Kahama MC
Ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa kushirikiana na Mtandao wa Malezi Taifa [TECDEN] na Shirika la ICs wamefanya kikao cha robo cha kujadili Utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ( PJT-MMMAM).Kikao hicho kimefanyika kwenye Ofisi ya Ustawi wa Jamii ya Manispaa hiyo huku Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Wa Shinyanga ikiwakilishwa na Bi. Lydia Kwesigabo ambaye ni Afisa Ustawi wa Mkoa.


